Skip to content
🤖 Chat with our bot about faith ☪️, life 🌍 & books 📖 Chat Now
Home » IJTIHAD NA TAQLID pdf book download for free swahili

IJTIHAD NA TAQLID pdf book download for free swahili

IJTIHAD NA TAQLID
  • Book Title:
 Ijtihad Na Taqlid
  • Book Author:
AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH
  • Total Pages
928
  • Book Views:
  • Click for the  

Warning: Undefined variable $post in /home/fastivgv/openmaktaba.fastwebcreators.com/wp-content/plugins/insert-php/includes/shortcodes/shortcode-php.php(60) : eval()'d code on line 2

Warning: Attempt to read property "ID" on null in /home/fastivgv/openmaktaba.fastwebcreators.com/wp-content/plugins/insert-php/includes/shortcodes/shortcode-php.php(60) : eval()'d code on line 2
PDF Direct Download Link
  • Get HardCover  
Click for Hard Copy from Amazon

IJTIHAD NA TAQLID – Sampuli

IJTIHAD NA TAQLID

MAANA YA SHARIA’HNA TASHRI’I

Neno Sharia’hkilugha maana yake ni ‘Njia inayopitwa sana kuelekea kwenye chanzo cha maji’ ambacho ni chanzo cha uhai wa kila kiumbe na vile vile a njia ilinyooka. Qur’animetumia mara kadhaa neno Sharia’hikiwemo katika aya zifuatazo:-

(لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًاۚ)

Likullin jaAAalna minkum shirAAatan waminhajan(Surat Al Maidah 5:48)

Tafsir: Kwa kila mmoja miongoni mwenu tumekujaalieni Sharia’h na njia iliyowazi.(hapa neno Shir`at limetumika kumaanisha njia,mfumo au mpangilio).

atika Qur’anpale Allah Subhanahu wa Ta’alaalipomwambia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salamkua:

(شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِۚ)

SharaAAa lakum mina alddeeni ma wassa bihi noohan waalladhee awhayna ilayka wama wassayna bihi ibraheema wamoosa waAAeesa an aqeemoo alddeena wala tatafarraqoo feehi(Surat Ash Shuraa 42:13)

Tafsir: Yeye (Allah) amekuwekea juu yenu Shara’a katika dini ile ile kama aliyomuwekea Nuh, na kama tuliyokushushia wewe (Muhammad), na tuliyomshushia Ibrahim, Musa na Isa ili kusimamisha Dini na msifanye mfarakano ndani yake.

Ingawa nimeitumia aya hii kwa ajili ya kufafanua maana ya neno Sharia’hlakini pia aya hii ni aya ya pili iliyowataja Ulul A’zmiwote kwa pamoja baada ya ya ile aya tuliyoiangalia mwanzo tulipozungumzia Ulul A’zmikatika Surat Al-Ahzab 33:7.

Hivyo kulingana na aya tulizoziangalia hapo juu tunaona kua Sharia’hmaana yake hua ni mfumo au njia ya kuelekea kuliko kusudiwa na Allah Subhanahu wa Ta’alaambae ndie muanzilishi na muumbaji wa kila kilicho hai. Vile vile tukiangalia katika mtizamo wa Fiqhbasi tunaona kua Sharia’hmaana yake ni njia iliyowekwa na Allah Subhanahu wa Ta’alakwa ajili ya kufuatwa na Bani Adam.

Tashri’imaana yake ni njia ya kuisimamia Sharia’h, hivyo kufanya Tashri’ihumaanisha kuweka au kufuata njia za kanuni na maelekezo ya mpangilio na mfumo ambao wahusika wanatakiwa kuufuata ipasavyo ili kuwapatia Bani Adammafanikio ya Maisha ya Duniani na Akhera.

Mukhtasarwa mfano wa mafanikio hayo hua yanaonekana wazi pale tunapoiangalia Hadithmaarufu iliyomo katika Sahih Muslimambayo hua inayojulikana kama Hadithya Jibril A’layhi Salaamisemayo kua:

Anasema Umar Ibn Khattab kua: ‘Siku moja wakati tukiwa tumekaa na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, ghafla alitokea mtu mmoja ambae alikua amevaa nguo nyeupee na nywele zake zilikua nyeusii, lakini hata hivyo hakuonekana kua ni mtu ambae alikua ni mwenye kutoka safarini. Na hakuna hata mmoja miongoni mwetu ambae aliekua akimjua mtu huyo.

Mtu huyo alikuja akakaa kitako mbele ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, kiasi ya kua magoti yake yakagusana na magoti ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, kisha akaiweka mikono yake juu ya magoti ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salamna kusema: ‘Ewe Muhammad! Hebu nielezee kuhusiana na Uislam.’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salamakasema: ‘Uislam ni kushuhudia kua hakuna Mungu isipokua Allah na Muhammad ni Mtume wake; na Kusali, kkah, na kufunga Ramadhani, na kuenda Makkah Kuhiji kwa mwenye uwezo.’

Yule mtu akasema: ‘Umesema ukweli’, hivyo nasi tukashangaa kua yeye ndie alieuliza suali na kisha yeye yeye ndie anaethibitisha jibu lake.’

Kisha akauliza, ‘Niambie kuhusiana na Iman.’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salamakajibu: ‘Ni kuamini juu ya Allah, na Malaikawake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na Qadar – uzuri wake na ubaya wake.’

Yule mtu akasema: ‘Umesema ukweli, sasa niambie kuhusiana na Ihsan.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salamakajibu: ‘Ni kumtumikia Allah kama kwamba unamuona, na kama humuoni basi kwa hakika yeye hua anakuona.’

Yule mtu akasema: ‘Umesema ukweli, sasa niambie kuhusiana na Saa ya mwisho.’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salamakajibu: ‘Yule aneulizwa hajui kitu kuhusiana na hilo kuliko yule anaeuliza.’

Yule mtu akasema: ‘Niambie kuhusiana na dalili zake.’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salamakajibu: ‘Ni pale wanawake watumwa watakapozaa mabibi zao; na utakapoona wanaotembea bila ya viatu, bila ya nguo, na mwanzo wa wachunga kondoo kushindaniana kujenga majumba marefu.’

Kisha yule mtu akaondoka, nami nikasubiri kwa muda mrefu. Kisha Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salamakaniuliza : ‘Jee unamjua ni nani yule aliekuja kuuliza masuali. Ya Umar?’

Nami nikajibu: ‘Allah na Mtume wake wanajua zaidi’, nae Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salamakasema: ‘Yule alikua ni Jibril. Alikuja kukufundisheni dini yenu.(Sahih Muslim)

Katika Hadithihii tunaona kua, wakati alipoulizwa kuhusiana na Uislam na Iman Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salamalijibu sehemu zinazoyajumuisha mambo hayo kwa pamoja, na alipoulizwa kuhusiana na Ihsan,basi tunaona kua alizungumzia kuhusiana na Tabia na Maadili. Hivyo, kulingana na msingi wa Hadithhii, Wanazuoni wa Sharia’hya Dini ya Kiislam wameigawa I’lmya mafunzo ya Sharia’hkatika sehemu tatu ambazo ni A’qai’d, Akhlaq na Ahqam.

(i) A’qai’d(Aqida): Haya hua ni mafunzo ya mambo ambayo ni lazima yafahamike na pia yanatakiwa yaaminiwe kwa kila Muislam. Mambo haya yanajumuisha ingi ya Iman kama vile, umoja wa Allah Subhanah wa Ta’ala, Sifa zake, Mitume wake, Vitabu vyake na mambo mengineyo.

I’lmya mafunzo haya hujulikana kama, I’lm al Aqaid.I’lmhii tutaiangalia kwa

undani zaidi mwishoni mwa sura ya tano.

(ii) Akhlaq(Maadili): Haya hua ni mafunzo ya mambo ambayo yanahusiana na maamrisho na ushughulikiaji wa Nafsina Tabia za Bani Adamkama vile uadilifu, ucha Mungu, ushujaa, usafi, busara, ustahmilivu, ukweli, uaminifu n.k kwa kuonesha namna gani Bani Adamanatakiwa awe. I’lmya mafunzo haya hujulikana kama, I’lm al Akhlaq.

Allah Subhanahu wa Ta’alakatika kutuonesha mfano wa Akhlaqanasema katika

Qur’ankwa kumuambia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salamkua:

(إِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ)

Wa-innaka laAAala khuluqin AAadhdheemin(Surat Al Qalam 68:4)

Tafsir: Na hakika, wewe (Ewe Muhammad) ni mwenye khuluq bora kabisa.

Anasema Abu ‘Ali Ahmad Ibn Muhammad Ibn Ya’qub Ibn Miskawayh katika kuielezea maana ya neno Khuluqambayo wingi wake ni Akhlaqkatika kitabu chake, kua : ‘Khuluqni hali ya Nafsiinayoipelekea kufanya vitendo bila ya kuhitaji haja ya kutafakari au haja ya kua na kusudio. Hali hii huweza kugawika katika sehemu mbili: Kwanza ni kua hali ya maumbile na hua ni sehemu ya tabia halisi ya mtu, kama vile kucheka sana kwa kila kitu kinachomfurahisha, au kuhuzunika kutokana na kitu chochote kibaya kitakacho mtokezea.

Hali ya pili ni ile yenye asili ya kulelewa na kufundishwa kikawaida, na ingawa inaweza kua ina asili ya kutokana na kutafakkar na pia kukusudia lakini hatimae hua ni sehemu ya tabia.’(Tahdhib Al Akhlaq)

Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Al Ghazal yeye anasema kuhusiana na Khuluqkatika kitabu chake cha Ihya Ulum Dinkua : ‘Khuluqni jina la hali ya kitu chenye asili ya kina na ithabati katika Nafsi, hali ambayo husababisha vitendo kutekelezeka kwa urahisi na kwa utaalamu bila ya kuwepo na haja ya kutafakari au kukusudia. Na inapofikia kiasi ya kua hali hii inazalisha ndani ya Nafsivitendo vizuri na vya kupendeza kutokana na mtizamo wa ufahamu na wa Sharia’hbasi hio hua ni Tabia nzuri; Na inapofikia kiasi ya kua hali hii inazalis Nafsi,basi hio hua ndio Tabia mbaya.

To read more about the Ijtihad Na Taqlid book Clickthe download button below to get it for free

or

Report broken link
Support this Website


for websites

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments

You are reading pdf file online

Loading PDF, please wait...
Error: The PDF file could not be loaded. Please try again later.
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x